chakarika

Monday 31 May 2010

Hawa ndiyo wapiga kura wenu CCM!!!?



Miaka nenda rudi tunaishi kwa matumaini ambayo hayapo. Je waziri Kapuya unasema nini kuhusiana muda mfanyakazi kazi kibaru unakoma baada ya muda gani ili kupata mkataba. Hawa wapiga kura wenu ninyi chama tawala wapo utumwani katika nchi yao. Ajira zao zinaanza asubuhi na kukoma jioni tena kwa muda usiokuwa na kikomo. Kifupi ajira inaanza asubuhi lakini haifahamiki muda wa kumaliza kazi.

Na hata hiyo asubuhi itategemea na saa ya utakayofika hapao kazini. Iwapo umechelewa basi nafasi siku hiyo nayo imetoweka. unatakiwa kujibidisha kufika kazini mapema ikiwezekana masaa mawili kabla kuanza kazi. Je CCM mpo hapo...kumbukeni mpo madarakani muda wa miaka thelasini na tatu kwa jina la CCM na kabla ya hapo kwa jina TANU.

Nini kipya mtakachotueleza safari hii

No comments:

Post a Comment