chakarika

Monday 31 May 2010

Ukivulia Nguo maji ni sharti kuoga mwili mzima




Iwapo tumekubali kuingia katika mfumo wa vyama vingi basi tukubali kutekeleza kila kitu na tuache visingizio ambavyo haviendani na mfumo wa demokrasia ya vyama vingi. Tukumbuke kuwa tulikuwa na mashirka ya umma tena mengine yalikuwa yakiendeshwa kwa ufanisi lakini tukasema serikali kazi yake ni kusanya kodi na siyo kufanya biashara na viongozi wetu wakahamua kuyauza mashrika yote, na mengine kufa kifo cha mende na pia kuuzwa kwa bei ya bure kama NBC.

Sasa tumeingie kwenye mfumo wa vyama vingi basi moja kwa moja tukubali kila kitu katika mfumo...kama hili suala la mgombea binafsi. Kwa sababu tukumbuke jamii yeytu sasa hivi inatakiwa kumshirikisha kila mpiga kura wetu ashiriki katika chaguzi mbalimbali, na siyo kila mpiga kura ni shabiki wa vyama vya siasa. Kuna wapiga kura ambao wangependa kupiga kura kwa mgombea binafsi. Na kwasababu hiyo basi mara nyingi wanashindwa kuitumia haki yao kupiga kwa kukosa mgombea binafsi....Inaendelea

No comments:

Post a Comment