chakarika

Sunday 30 May 2010

Soka ya Tanzania itabadilika kwa kucheza na Timu ya Taifa-Brazil ndani dakika tisini!?


Mtazamo wangu hupo tofauti kabisa na chanzo halisi ya matatizo ya soka ya Tanzania...Tukumbuke kuwa Brazil kiuchumi wapo juu yetu kidogo ingawa kimsingi ni wenzetu katika masuala ya mambo ya uchumi. Je wamewezaje kuweza kuwa na mafanikio ya katika soka kuliko sisi! Imekuja timu ya Taifa ya Ivory Coast imetusaidia nini? Je ni kweli baadhi ya wachezaji wetu walionekana katika runinga ya SKY na jingine zenye majina makubwa. Hivi ni kweli tunachohitaji ni kucheza na timu kubwa za Taifa!?

Kimsingi hizo pesa zilizolipwa kwa Brazili ili kucheza na timu ya Taifa ya Tanzania zingeweza kuwapeleka kusoma soka wachezaji wastaafu ya timu ya Tanzania kozi za muda mrefu na pia marefa wale wote wenye nia ya kufanya hivyo huko Brazil. Mimi nachoona tunachokosa hapo ni wataalamu wa kuendeleza vipaji, viwanja vya soka safi na salama, marefu wenye mafunzo tangu wakiwa wadogo na vifaa vya michezo. Sina sababu ya kuzungumzia viongozi wa vyama vya michezo kwa sababu hayo yatajitengeneza yenyewe iwapo tukiweza kuwa wataalamu wa soka wenye ujuzi wa kisasa.

Hivi sasa vipaji vya soka Tanzania vinajivumbua vyenyewe bila ya usimamizi wa kiutaalmu matokeo yake. Maumbile ya wachezaji wetu wengi hayaendani na nafasi wanazocheza uwanjani. Imefikiwa wakati viongozi wa soka na mashabiki huwa wanakimbilia kuwalaumu wachezaji kwamba wameongwa baada ya mechi kuwa wamecheza chini ya kiwango bila kuangalia na hao wachezaji kujitambua nafasi wanazhocheza haziendani na wao walivyo kiumbo na urefu pia....

Uzoefu wa mechi za majaribio ni kujifunza, tulipocheza na Misri na Ivory Coast nini tulichojifunza hapo!? Cha zaidi kilichotokea ni aibu tuu kufungwa magoli matano Misri. Hamasa ya wachezaji haitapatikana kwa kucheza na timu kubwa kama hii ya Brazil. Hii naweza kufananisha Mtoto anayetambaa akaharakishwa kukimbia kabla hata miguu ya huyo mtoto kutengemaa kuweza kuimilia uzito wake binafsi. na hata hao wanaosema Tanzania kwa kucheza na Brazil basi itakuwa imefahamika katika ramani ya soka ya dunia. Mimi nategemea kufahamika kwetu katika ulimwengu soka ni kwa kufungwa magoli ya aibu katika ulimwengu wa soka.

Soka yetu ina matatizo makubwa sana yanayotokana na utaalamu zaidi kuliko tunavyofikria. Leo hii nchi kama Ghana, Cameroon, Nigeria, Senegal na Ivory Coast. Wamewezaje kufikia hapo walipo. Nilitegemea hili ndiyo vitu TFF na wadau wengine wa soka wangejadili kwa kina ili kupata jibu la kudumu. Soka ni sayansi na sisi tupo nyuma sana kitaaluma. Hata hawa wataalamu tuliyonao hivi sasa wamesomea hiyo elimu wengine hata kabla ya mobile phone Technology kufika Tanzania.

Kimsingi sisi ni watawala wazuri kwa mambo ya muda mfupi kuliko mikakati ya endelevu ya muda mrefu. Tungetafakari vizuri hicho kiwango cha pesa kinachotumika kuileta Brazil ingeweza kuleta mageuzi ya kweli katika soka kwa kuwapeleka wachezaji wastaafu waliwahi kucheza timu ya Taifa na vijana ili waweze kusoma kozi ya soka za kisasa kwa nchi kama hiyo Brazil. Hayo maarifa wangeweza kwenda sasa kushirikia kikamilifu kuvumbua vipaji na maarifa watakayokuwa mwamejinza. Hivi Leo hatuna wachezi warefu katika soka na ukweli unafahamika unapokuwa mrefu kuna sifa kama mchezaji.

Maumbile ya wachezaji hayawezi kujitambua yenyewe ni sharti kuwe wataalamu wa hiyo nyanja walisomea elimu kisasa ndiyo waweze kufmumbua. Makocha wa kigeni ni muhimu kuwa kwa timu ya Taifa lakini suala kubwa ni lilelile. Kocha mzuri wachezaji siyo wazuri kwa sababu mchezaji wa timu ya Taifa anapoitwa timu ya taifa ni vyema kwa huyo mchezaji kuwa tayari kisoka lakini siyo hawa tulikuwa nao. Wengi wao bado wanahitajika tena kufundishwa hata jinsi ya kufnga goli. na hiyo siyo sifa mchezaji anayeitwa kuja kuchezea timu ya Taifa. Kocha wa Timu Taifa anakuja kutengeneza patern ya uchezaji siyo kukufundihsa jinsi ya kumiliki mpira.

Iwapo mtu yeyote angependa kushiriki huu mjadala anakaribishwa....

1 comment:

  1. Kweli kabisa Mzee.....hata baadhi makipa wetu ni wafupi kulinda lango za timu zetu

    ReplyDelete