chakarika

Monday 31 May 2010

Liyumba Amefungwa Jela au Walalahoi wamefumbwa Akili!!!?


Nikitafakari kwa kina naona ni wengi wapo kama Bwana Liyumba katika hizi tuhuma lakini bado sheria haijachukua mkondo wake. Kuna suala la rada hapa la ufisadi wa rada hapa na mabilioni ya EPA yaliyoingia mifukoni kwa mimi nawaita watu wenye akili kuliko sisi sote watanzania. Maana wametenda uhalifu lakini ndiyo kwanza wanaishi kama peponi na sheria na vyombo vyote vya dola vipo vikiwatazama...

Mimi Mcharikaji kuganga njaa na elimu yangu duni siwezi kupambana nao. Je na hao viongozi tuliowapigia kura wanawakilisha hao waahailfu maarufu siku hizi MAFISADI au wanatuwakilisha sisi!!?. Je kuhukumia kifungo kwa Bwana Liyumba ni kwa ajili ya kuturidhisha sisi walalahoi kuwa serikali inafanya juhudi ya kufuata utawala wa sheria. Uchaguzi mkuu bado miezi takribani mitano mpaka kufanyika au hii hukumu inaendana na mahitaji yetu au mahitaji ya hao watawala kupigiwa kura halafu turudi kama kawaida mahakamani kukata rufaa, Bado inaendelea.........

No comments:

Post a Comment